ZIJUE HASARA ZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI KATIKA ENEO ULILOPO

Vijana wengi tunasita kushiriki uchaguzi katika mazingira yetu kwa kutokujua hasara zitokanazo na kufanya hivyo....

UCHAGUZI mara nyingi hufanyika katika ngazi yoyote ile ambapo kuna jamii fulani ya watu,Ni wazi kuwa kundi la watu huwa linahitaji kuwa na Kiongozi, Maana hata wanyama mbugani nao pia wana Uongozi ambao unawaongoza katika mawindo wawapo nyikani..

Katika jamii inayohitaji maendeleo, Uchaguzi una nafasi kubwa sana katika kusimamia mipango na mikakati mbalimbali ya kijamii.Tunapozungumzia maendeleo katika jamii tunagusa moja kwa moja maendeleo ya mtu binafsi, maana mtu huwezi kuwa na maendeleo kama jamii inayokuzunguka haina maendeleo,,

Kwakuwa maendeleo ya jamii humgusa mtu moja kwa moja hivyo basi tunaona wewe kama kijana Unayo nafasi kubwa sana ya kuamua  maendeleo katika jamii inayokuzunguka, Maana ya kuwa msomi ni kukufanya utambue kuwa una nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii yako yawe ni mabadiliko chanya au hasi

Linakuwa ni jambo la kusikitisha sana unapomkuta kijana msomi anasema kuwa "kura yangu moja haina madhara "

HIZI NI MIONGONI MWA HASARA ZA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI KATIKA JAMII YAKO!!!!

1.Utapata kiongozi ambaye hukumuhitaji maana hukupiga kura,Ungemuhitaji ungempigia kura.

2.Utakuwa ni mtu wa kulalamikia mfumo unaokuongoza.

3.Inakushushia hadhi yako kama mtu msomi na anayejitambua, maana halisi ya usomi ni kuamini kuwa una nguvu ya kuleta mabadiliko.

4.Unawaumiza wengine, maana mfumo unabadilishwa na jumuiya nzima ya watu ukiwemo na wewe mwenyewe.

5.Unaathirika kisaikolojia, maana utakuwa ni mtu wa kulaumu viongozi wako na pia unakosa kujiamini kama kijana mwenye nafasi ya kuleta mabadiliko.

Vijana tunapaswa kutambua nafasi yetu katika maendeleo ikiwemo kushiriki chaguzi mbalimbali zinazotokea katika jamii zetu.. Maana jamii inayokua inahitaji viongozi bora, Viongozi ambao watasimamia vyema mipango na mikakati ya maendeleo katika jamii ambayo yanawagusa moja kwa moja wanajamii wa eneo hilo


AMKA SASA NENDA KAPIGE KURA, SHIRIKI UCHAGUZI, UNA NAFASI  KUBWA SANA YA KULETA MAENDELEO, 

Comments

  1. Exactly bro....uchaguz ni muhimu sana MTU kushiriki

    Tumepokea

    ReplyDelete
  2. Kupiga kura ni haki ya msingi.
    Kumchagua kiongz bora ni jambo la msing zaid

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

"Fahamu zaidi..."