Vijana wengi tunasita kushiriki uchaguzi katika mazingira yetu kwa kutokujua hasara zitokanazo na kufanya hivyo.... UCHAGUZI mara nyingi hufanyika katika ngazi yoyote ile ambapo kuna jamii fulani ya watu,Ni wazi kuwa kundi la watu huwa linahitaji kuwa na Kiongozi, Maana hata wanyama mbugani nao pia wana Uongozi ambao unawaongoza katika mawindo wawapo nyikani.. Katika jamii inayohitaji maendeleo, Uchaguzi una nafasi kubwa sana katika kusimamia mipango na mikakati mbalimbali ya kijamii.Tunapozungumzia maendeleo katika jamii tunagusa moja kwa moja maendeleo ya mtu binafsi, maana mtu huwezi kuwa na maendeleo kama jamii inayokuzunguka haina maendeleo,, Kwakuwa maendeleo ya jamii humgusa mtu moja kwa moja hivyo basi tunaona wewe kama kijana Unayo nafasi kubwa sana ya kuamua maendeleo katika jamii inayokuzunguka, Maana ya kuwa msomi ni kukufanya utambue kuwa una nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii yako yawe ni mabadiliko chanya au hasi Linakuwa ni jambo la kusikitisha sa...