KUELEKEA SUASO ELECTION 2020/2021


Pata kumfahamu Frank Moses ambaye ni mgombea
mwenza wa ndugu Abdon Theonest katika kiti cha urais wa SUASO. Ndugu Frank Moses alizaliwa tar 27 julai 1997 mkoani Rukwa Tanzania,Alihitimu elimu yake ya msingi mwaka 2011 katika shule ya msingi Tunduma iliyopo katika wilaya ya Momba mkoani Songwe,Akafanikiwa kujiunga na sekondari ya wavulana ya songea(Songea boys) kwa masomo ya O-level 2012-2015.Baadaye alifanikiwa kujiunga na shule ya Same sekondari iliyopo mkoani MOSHI kwa ajili ya masomo yake ya A-level kwa mchepuo wa CBG 2016-2018.Baada ya kuhitimu kidato cha sita,alipata nafasi ya kujiunga na Jeshi la kujenga taifa kwa ajili ya mafunzo ya Uzalendo na Ujasiriamali katika kikosi cha mlale mkoani Ruvuma (842KJ) kabla ya kujiunga na chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ambapo anachukua kozi ya Kilimo, uchumi na biashara.
   HISTORIA YAKE YA UONGOZI 
Class monitor- Songea boys (2012) 
Domitory leader-Songea boys (2013)
Makamu mwenyekiti serikali ya wanafunzi Songea boys (2014)
 Kaimu Mwenyekiti serikali ya wanafunzi Songea boys (2015)
Mwenyekiti serikali ya wanafunzi Same sekondari (2017) 
 Section trainer(ST) mlale jkt,COY D (2018) 
Mbunge wa kihonda block 'A' -SUA (2019/2020)
 Ni kijana aliye na mtazamo chanya katika jamii yake,Vilevile anaonekana mtu bora katika Uongozi katika kila jamii inayomzunguka. Akiwa pamoja na Abdon Theonest katika kuwania nafasi ya URAIS SUASO 2020/2021,Wamejipanga katika kuhakikisha wanashirikiana na WanaSUASO katika kuhakikisha changamoto zinatatuliwa ili kuifanya jamii ya SUA kuwa sehemu bora ya kuishi na vilevile mahali pa kupata elimu iliyo bora ambalo ni lengo la kila MwanaSUASO..Wanahitaji ushirikiano wako kwa kuwapigia kura kama kauli yao isemavyo 'TEAM WORK,TRANSPARENCY & 
ACCOUNTABILITY'
 BAADHI YA MATUKIO MBALI MBALI AKIWA SEHEMU MBALIMBALI KAMA KIONGOZI
Team Leader AEA

  • Akiwa na viongozi wake pamoja na wageni SAME Sekondari 2017

''Same is not THE SAME''😃
SAME SEKONDARI
 


   
Songea Boys 2014
    


Comments

  1. Historian ya uongozi inakwenda kubadilika na kuwa mtu mzito suaso✌️✌️✌️

    ReplyDelete
  2. You deserve kura yangu niyako

    ReplyDelete
  3. Wanasuaso sijui wanahitaji nini tena Hawa ndio viongozi bora kabisa

    ReplyDelete
  4. Kura yangu chukuaa 🙋🙋

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

"Fahamu zaidi..."