Kwanini Leo Messi anataka kuondoka Barca...
Mchezaji wa kimataifa kutoka Argentina Leo Messi 33
anayekipiga katika klabu ya Barcelona nchini Hispania kwa mara kadhaa amekuwa akihusishwa kutaka kuondoka klabuni hapo,Moja ya vitu vinavyotajwa kama sababu ya yeye kutaka kuondoka ni baada ya timu hiyo kudorora sana katika msimu huu uliokwisha malizika tayari, Ikumbukwe kuwa klabu hiyo yenye makazi yake Catalonia imeonesha uwezo mdogo tofauti na matarajio ya wengi katika msimu huu ukilinganisha na misimu yote ambayo imekuwa ikifanya vizuri.
Leo Messi amenukuliwa mara kadhaa akilaumu uongozi wa klabu hiyo ya dimba la Camp nou, kwa kushindwa kuongoza vizuri timu hiyo ikiwemo yeye mwenyewe kutokuwa na maelewano mizuri na kocha wake Quique Setien ambaye amefukuzwa kibarua tayari klabuni hapo.
Kushindwa kuchukua kikombe cha ligi (LA LIGA 2019/2020) pamoja na kuondoshwa vibaya katika robo fainali ya michuano ya UEFA champions league baada ya kipigo kikali cha bao 8-2 kutoka kwa Bayern Munich ni miongoni mwa vitu vilivyozidi kumchochea nyota huyo kutaka kuondoka klabuni hapo...Nini maoni yako kwa mchezaji huyo?


Aende man city tu patamfaa
ReplyDeleteAende Manchester City au Borrusia Dortmond kutamfaa zaidi
ReplyDeleteAsikate tamaa yeye ni mchezaj mkubwa
ReplyDeleteMimi naitwa bikery taito music mesi niriaondoke tu baselona mimi nimshabiki watimu iyo lialia
ReplyDelete