Kwa nini unashauriwa kutazama filamu,sinema,Movie??
Filamu ni miongoni mwa sanaa bora
kabisa katika sanaa za maonyesho, Mara nyingi huwa zinahusisha visa mbali mbali ambavyo vinajumuisha maisha yetu..Labda nikukumbushe kuwa upo katika dunia ambayo ina kila aina ya mambo ambayo hata ungetaka kuyapitia yote, hutaweza kuyamaliza, Maisha yetu yanahitaji furaha, mafundisho na faraja pia..
Nguvu kubwa iliyopo katika filamu ni kukupitisha wewe mtazamaji katika visa na maisha fulani ambayo pengine kwa muda wako wa kuishi hapa duniani usingeweza kukutana nayo kabisa. Filamu zina uwezo wa kukupeleka msituni bila hata wewe kujua, zina uwezo wa kukuliza na kukufuta machozi pia, Zina uwezo wa kukukatisha tamaa na kukupa nguvu tena Haya ni baadhi ya mambo ambayo tunakutana nayo pia kila siku katika maisha
Lakini pia kupitia filamu unapata kujua namna watu wa sehemu mbalimbali duniani wanavyoishi, Unajifunza utamaduni wao,lugha zao ambapo sehemu zingine hukuwa na uwezo wa kufika.
Maisha yetu yanaongezewa ladha nzuri sana tunapotazama filamu, Maana tunapata mafundisho mbalimbali(Experience) ambayo pengine tusingeyapata sehemu yoyote ile.
Wewe unapendelea kutazama filamu zipi?


Swahili movie , bible stories
ReplyDelete